My Favourite Site

Blogger Tricks

widgeo.net
Designed by Jeymodel Fashion. Powered by Blogger.
Wednesday, October 22, 2014

MACHOZI YA HOYCE TEMU YAITAFUNA MISS TANZANIA!


MACHOZI YA HOYCE TEMU YAITAFUNA MISS TANZANIA!


Wakati kamati ya Miss Tanzania ikijiandaa kutoa msimamo kuhusiana na kashfa ya Mrembo wa Mwaka 2015 Sitti Mtemvu katika hotel ya JB leo itakapozungumza na waandishi wa habari,Hoyce Temu mshindi wa Miss Tanzania mwaka 1999 alimwaga machozi mwaka 2007 mara baada ya jopo la majaji wa shindano hilo kumtangaza mnyange mwenye asili ya kihindi,Richa Adhia,kuwa ndiye Miss Tanzania aliyestahiki na kurithi mikoba ya mtangulizi wake mwaka 2006 Wema Sepetu!
Alisema kamwe sitarudi kutazama kujihusisha na Miss Tanzania kwa vitendo hivi vya ubabaishaji vinavyofanywa na waratibu wa shindano hili na kwa mfumo huu Tanzania hatuwezi kamwe kupata mrembo atakayeweza kufunika Miss World iwapo hakutakuwa na mabadiliko.
Aliendelea kusema,kiukweli kabisa Richa akustahili kushinda Taji hili la Miss Tanzania,amependelewa wazi na waandaaji,kwani kulikuwa na warembo wenye vigezo vingi kumshinda lakini wenye rangi stahiki ya kuiwakilisha nchi.
Mambo haya yalianza zamani jamani ni wakati sasa wa Serikali kuchukua maamuzi ngumu kuyanusuru!


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: MACHOZI YA HOYCE TEMU YAITAFUNA MISS TANZANIA! Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top