My Favourite Site

Blogger Tricks

widgeo.net
Designed by Jeymodel Fashion. Powered by Blogger.
Sunday, July 20, 2014

POCHI YA MWANAMKE


Pochi ni sehemu muhimu sana katika maisha ya mwanamke. Pochi zipo za aina, rangi, ukubwa na matumizi mbali mbali. Ni nadra sana kukutana na binti au mama anayetembea bila pochi, na kwa wengine maisha yao yote wanatembea nayo kwenye pochi
Kuna vitu muhimu ambavyo ni lazima kila mwanamke akumbuke kutembea navyo kwenye pochi, na kuna vingine ni vyema kuwa navyo lakini sio lazima.
Muhimu
1. Pini
2. Sindano na uzi
3. Vifungo
4. Dawa yoyote ambayo unaitumia na kuihitaji
5. Kitambulisho
6. Pedi
7. Kalamu na notebook
Ukipenda
1. Perfume
2. Lip shiner / lip stick
3. Poda
4. Kitana
5. Khanga / mtandio
6. Kadi ya benki
7. Sandals kama unavaa viatu virefu

Mara nyingi wanawake tumekuwa tukijichukia na kujiona si wazuri wala hatupendezi kwa kuangalia muonekano wa nje. Unajiangalia na kujilinganisha na wengine na kuishia kuona mabaya (usiyoyapenda) na kuacha kuona jinsi Mungu alivyokuumba vyema na kukubariki. Utaona kuwa hauna nywele nzuri kama fulani, umenenepa/ kukonda sana, hauna elimu kama wengine, haujaolewa na mengine mengi.
Tambua hakuna mwanadamu aliye mkamilifu bali Yesu Kristo Bwana wetu ndiye atukamilishaye. Hivyo ulivyo ni wa thamani sana mbele zake na anakuhitaji uache kuangalia madhaifu yako bali umwangalie yeye ili aweze kukutumia. Jenga tabia ya kuhesabu baraka zako kila siku na utaona jinsi maisha yako yatakavyo badilika. Jione vile Mungu anavyokuona na acha kutumia vipimo vya wanadamu kutambua thamani yako.
Hivyo ulivyo Mungu anataka kukutumia, kwa elimu uliyonayo, kazi uliyonayo, nafasi yako hiyo hiyo uliyonayo, Mungu anakuhitaji. Unaweza kudhani kuwa ungekuwa na elimu zaidi, nafasi kubwa zaidi kwenye jamii, umeolewa, unakarama kama ya fulani basi ungemtumikia Mungu. Ukweli ni kwamba hivyo ulivyo unahitajika shambani mwa BWANA, kwa karama aliyokupa (kila mmoja wetu amepewa, nitafundisha juu ya hili siku zijazo). Anza sasa kumtumikia Mungu na utaona jinsi gani utabarikiwa na kuinuliwa zaidi na zaidi.
1 Korintho 15:10 Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo; na neema yake iliyo kwangu ilikuwa si bure, bali nalizidi sana kufanya kazi kupita wao wote; wala si mimi, bali ni neema ya Mungu pamoja nami.”
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: POCHI YA MWANAMKE Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top