My Favourite Site

Blogger Tricks

widgeo.net
Designed by Jeymodel Fashion. Powered by Blogger.
Monday, August 25, 2014

SAFARI YANG YA KUWA MWANA MITINDO ILIPO ANZIA NA MAMBO YA MSINGI AMBAYO ILINIBIDI NIJFUNZE

NAKUMBUKA SAFARI YANG YA KUWA MWANA MITINDO ILIPO ANZIA NA MAMBO YA MSINGI AMBAYO ILINIBIDI NIJFUNZE MARA MOJA PINDI NILIPO FANYA UWAMUZI WAKUWA MWANA FASHION AU MODEL


Kwa majina yang naitwa JUSTUS JACKSON JEREMIA MASHENENE (jeymodel) Nilipoamua kuingia kwenye fani ya model kwa kweli sikuwa na mengi sana zaidi ya kujifunza namna ya kutembea na namna ya kuweka poz na kujua model anatakiwa aweje anapokuwa katika poz au runway..

 Kablay ya kuendelea tapenda niwambie kitu kimoja nijuacho mie juu ya model. Model ni mtu waaina yeyote ile awe mzee, au kijana, mtoto wote wanafaa kuwa model kwan yeyote anae wakilisha kituchochote uyo nimodel tiyal.

 Mama yangu ni mlez wa kituo cha watoto cha kuleana muda mwing uwafundisha namna ya kuish na kuwa wabunifu katika maisha.  Katika kukua kwangu nimejifunza mengi toka kwake mojawapo likiwa ni hili.
  
Mpaka sasa nimeshashiriki maonyesho yapatayo ma nne katika fashion na mengi mengine yanakuja.
Maonyesho yote hayo yamekuwa changamoto kwangu kwa vile unakutana na akili tofauti zifanyazo ubunifu tofauti,Ila kwa sasa nimeamua kuwa na Agencey ya MODELS 

                                HII HAPA CHINI INAYOONYESHA UBUNIFU WANGU,

            

         

Baadhi wa wabunifu wa mitindo ambao nimewahi kuzungumza nao iwe katika mahojiano maalumu au hata katika mazungumzo ya kawaida tu wanasema sio lazima mwanamitindo au  mbunifu wa mitindo kwenda shule na kusomea chochote katika fani hii. 

Yaani mtu anaweza kuamka tu asubuhi akasema anataka kuwa mbunifu au mwana mitindo na akaanza kufanya hivyo.


                                           

  Si kweli kwamba unaweza ukaamka asubuhi na kuamua kuwa mbunifu wa mitindo,haya si maji ya kunywa kila mtu anaweza kunywa…ni suala la kutumia maarifa zaidi kuliko elimu au utundu.
Wagunduzi wengi wakubwa duniani walitumia maarifa zaidi kuliko elimu,maarifa kwa maana ya kuzaliwa nayo na si kufundishwa.
 Aliyegundua ndege alitumia maarifa bali anaesomea uhandish au urubani leo hii anatumia elimu.
Huwezi ukakurupuka na kuamua kuwa mbunifu,mbunifu wa kweli hutenda kweli…

Mimi ni mwana mitindo tena niliozaliwanao ndio maana katika maisha yangu imekuwa rahisi kwangu kufanya  yote isipo kuwa uchoraj graphic designing/cartoons/paintings na vinginevyo. Ila kuna wachoraj.
Wapo wabunifu wengi wazuri na wakubwa duniani ambao si wachoraji.
 Nami ninatamani sana kuwa mchorajina,ila kwa sasa ni kuelekeza wachoraji au washonaji wanafanya kaz yang.…natamani ningekuwa mchoraji kwan ingenirahisishia sana kazi yang.


Ni ushauri wa msingi ambao ningependa kuwapatia kwa mtu anayetaka kuingia katika fani ya ubunifu wa mitindo hivi leo hapa Tanzania kwa mfano?

                               

Kama ni mwamitindo au mbunifu wa kweli basi na atumie uwezo wake wote bila kukata tamaa huku akiweka nia nafsini mwake kwamba amezaliwa ili ashinde. Akili yako inapokwambia huwezi basi kufanikiwa kwako ni ndoto.

Ubunifu wa mitindo unakwenda sambamba na kitu ambacho wenzetu wanakiita “inspiration”.Kwa upande wang napata ‘inspiration’ kutokana na mazingira yanayonizunguka ‘nature’.Naweza kupata idea toka kwa wanyama,ndege,samaki,nyumba,majani,milima na vingine vingi.
 Ipo dhana kwamba kila kitu kinachotoka magharibi (everything from west) au nchi za Ulaya na Marekani ni bora kuliko vya kwetu.


Ni kweli vipo vingi toka magharibi ambavyo ni bora ila si kweli kwamba vyetu havifai. Ndani ya bara la Afrika kuna ubunifu wa hali ya juu sana nadhani tunachohitaji kufanya ni kuongeza ubora wa bidhaa zetu(quality),kupunguza gharama za uzalishaji ili mnunuzi amudu bei, kujiamini na kufanya kazi kwa bidii zetu zote pia tuache kuwaza na tuanze kufikiri.

Ni wazi kwamba kiasi kikubwa dhana hii inaathiri soko la wabunifu wetu.Kwa mfano mtu anasema yeye ni mwana mitindo au mbunifu lakini anachokifanya ni kilekile kinachofanyika Ulaya na Marekani ila pengine anatumia kanga/kitengeau kuchukua hiki na kile toka huko na kuviunganisha pamoja.Huku ni kudumaza ubunifu na kukomaza uigaji matokeo yake ni kukosa ‘identity’.
Nadhani ni wazo zuri kuendeleza kilicho chako ndani ya nchi yako.




Bila shaka yapo mambo mengi sana ambayo umeshajifunza tokea uingie katika fani ya ubunifu wa mitindo.Je,ni mambo gani ambayo unadhani ungeyajua kabla hujaingia katika fani hii pengine yangebadilisha kabisa mtazamo wako katika fani hii?

 Ndani ya fani ya kuwa mwana mitindo nimeshajifunza mengi kwa mfano kutokata tamaa,umuhimu wa kutumia akili za ziada na kwamba maendeleo ya mwanadamu hayatokani na rangi yake au vinginevyo bali ni maamuzi yaliyo kichwani mwake yaliyo katika mpangilio na mwelekeo ulio sahihi.


Ni jambo au mambo gani ambayo ungependa watu wayaelewe kuhusu fani ya ubunifu wa mitindo ambayo unahisi hayaeleweki hususani miongoni mwa watu ambao sio wabunifu wa mitindo?

 Ubunifu si rahisi kama wengi wanavyodhani, huwa naona sehemu mbalimbali za ushonaji zikiwa zimeandikwa ‘……fashion designer’.lakini kinachofanyika pale si ubunifu bali ni uigaji.

Kwa bahati mbaya wengi hudhani hata kuiga ni kubuni. Jambo lingine ambalo halifahamiki vizuri ni ile hali ya kudhani nguo ya kununua dukani ni ghali zaidi kuliko unayoshonewa.Pengine hii inachangiwa na kiwango duni cha nguo unayoshonewa kuliko unayonunua dukani na hii ni changamoto kwetu ili tuongeze viwango vya ubora unaoenda sambamba na dunia inavyotaka.Jambo hili linawezekana kwa sababu akili ni zilezile,mashine ni zilezile labda tofauti ni mazingira.


KWA LEO NAOMBA NIISHIE APA ILA ENDELEA KUWA NAMI KUJUA ZAID YA HISTORIA YANG.  
Asanten sana na niwashukuru kwa kupoteza muda wenu na kusoma yaliyo jeymodelfashion.
MUNGU AWE NA WEWE. 

TEGEMEA MAMBO MENG KUPITIA JEYMODEL FASHION USUSANI WALE WAPENDAO FASHION KM MIE.

sehemu ya pili


Hivi sasa ninamiliki kampuni au JEYMODEL FASHION iliyoko chin ya AB ENT'S. naweza kunieleza kidogo kuhusu malengo haswa ya JEYMODEL FASHION na ilikuwaje nikaamua kuanzisha JEYMODEL FASHION pamoja na changamoto nilizokabiliana nazo nilipokuwa naanzisha hii kitu?

JEYMODEL FASHION ikiwa chin ya AB ENT'S ni kampuni iliyojaa ubunifu wenye mwelekeo na mtazamo wa kimataifa. Ni kampuni inayokubali kwamba dunia sasa ni kijiji na kwamba penye nia siku zote pana njia.

Wakati naanzisha kampuni hii nimekumbana na changamoto nyingi zikiwemo kutojiamini.

Hivi sasa ulimwengu mzima unapambana na kitu kinachoitwa “Uharibifu wa mazingira”. Wanamitindo wengi wa wanakabiliwa na changamoto ya kushiriki kikamilifu katika kuhakikisha kwamba uharibifu wa mazingira unakuwa wa kiwango cha chini kabisa. Mimi kama mwanamitindo hapa Tanzania nakabiliana.

Uhifadhi wa mazingira ni jambo muhimu sana kwa kizazi kilichopo na kijacho,kwa kuzingatia hili kampuni yang inahakikisha hatutoi mifuko ya nailoni/plastiki kwa wateja wetu bali ya makaratasi maalum au vitambaa. Pia tupo mbioni kwa kushirikiana na kampuni nyingine itengenezayo vikoi kuanza kutengeneza nguo zitokanazo na pamba isiyo na kemikali (organic cotton) ili afya ya mvaaji isiwe hatarini.

Wateja wako ni kina nani hasa ni wale wapendao kupendeza huku wakiwa katika mwonekano tofauti kimavazi. Ni wa rika mbalimbali wanaoheshimu na kuelewa nini maana ya fashion.Wanatofautiana kimapato kwani wapo wamama wa nyumbani,mabalozi hadi mawaziri. Nawaheshimu sana watu hawa kwani wao pia wanatumia akili kuchagua mavazi sahihi kwao.

Kazi yakng na pengine maisha yang binafsi yamenipa nafasi ya kusafiri katika sehem mbalimbali hapa ulimwenguni. Katika kutembelea sehemu hizo na katika kulinganisha,kwa mfano,fani ya mitindo katika nchi hizo na hapa kwetu, kunasehem ambazo nimeona na kusema hili ni zuri na sisi pia tunaweza kuliiga na kulileta hapa nchini?http://www.facebook.com/jeymodelfashion

Hapa kwetu mambo ya fashion na ubunifu wa mavazi bado ni fani changa sana yaani kama ni mtoto basi ndio kwanza anatambaa. Wenzetu wa ulaya, marekani na nchi zilizoendelea wameanza karne nyingi zilizopita na kwa vyovyote vile wako mbele yetu.Kuendelea kwao hakutakiwi kuwa kikwazo kwetu bali changamoto.

Ubunifu tunao kwa karne nyingi zilizopita ila tatizo letu ni kutojiamini na kutoweka ubunifu wetu katika kumbukumbu pia kutoutumia katika matumizi ya kisasa yanayoendana na dunia ya leo. Mambo ambayo nimeyaona na kuyapenda toka kwao ni pamoja na;
ubunifu wa mavazi ni biashara inayoweza kuwa kubwa sana iwapo utaamua iwe hivyo.
nchi za wenzetu muda ni mali wakati sisi muda ni jua kusogea,wenzetu wawapo kazini hawatakiwi kusikiliza au kupokea simu wakati kwetu usishangae ukaitwa mnyanyasaji
pale unapomkataza mtu kufanya hivyo.
Wakati watu duniani wanaishi kwa kutumia maarifa,sisi bado tunatumia mazingira na ndio maana miaka hamsini baada ya uhuru bado tunasubiri mvua inyeshe ili tupate umeme, ni mambo ya ajabu kabisa!

Kwa wenzetu umaliziaji (finishing) ni muhimu sana ila kwetu bado kitabu kinauzwa kwa kuangalia jalada. Pengine hii inachangiwa nauchanga wa hii fani hapa kwetu.

Bara la afrika lina nafasi nzuri katika soko la nguo duniani kwa vile tunao ubunifu wapekee ambao bado haujasambaa. Tunachohitajika kufanya ni ni kuuweka katika katika sura ya kidunia ili wavaaji wawe wanadunia na si waafrika pekee.

Kama sikosei kazi ya fashion na ubunifu wa mitindo ni kama haina kikomo. Hata ukiwa mapumzikoni unaweza kuona kitu fulani cha ki-mtindo kikakuvutia na kukufanya uwaze na kuwazua.

Pamoja na hayo bila shaka kuna wakati napenda kupumzisha akili na roho na kuwa mbali na ulimwengu wa mitindo. Nikiwa mapumzikoni uwanapenda kufanya mambo haya, kusikiliza mziki, kusoma habari za watu mashuhuri waliofanikiwa maishani,kujua zaidi kuhusu wabunifu mashuhuri na wakubwa duniani,kulala vizuri,kufanya mazoezi n.k.

Welcome to Official Page, ® MODELNG FOR RUNWAYS, CATWALKS, DESIGNING, & TV COMMERCIALS Fashion Photographer, Portrait & Advertising Photographer http://www.facebook.com/jeymodelfashion

Asante sana kwa muda wako msomaji naomba ukalibu wako kila wakati...

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: SAFARI YANG YA KUWA MWANA MITINDO ILIPO ANZIA NA MAMBO YA MSINGI AMBAYO ILINIBIDI NIJFUNZE Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top