My Favourite Site

Blogger Tricks

widgeo.net
Designed by Jeymodel Fashion. Powered by Blogger.
Sunday, August 3, 2014

TAARIFA MPYA KUHUSIANA NA ZILE SHOWZ ZA USIKU WA MWAFRIKA ZILIZO FANYIKA JIJINI MWANZA.

TAARIFA MPYA KUHUSIANA NA ZILE SHOWZ ZA USIKU WA MWAFRIKA ZILIZO FANYIKA JIJINI MWANZA.


Kwa Wakazi wa Jiji la Mwanza watakuwa wanajiuliza Maswali mengi kuhusiana na ile Show ya African Night (Usiku wa Mwafrika) ambayo imefanyika tarehe 01.08.2014 Katika Ukumbi wa Serengeti pale JB Belmont Hotel na Siku ya tarehe 02.08.2014 pale Buzuruga Plaza.

Sasa iko hivi, Kamata huu Mtonyo kutoka jeymodel fashion ameshuhudia Mpango mzima kuhusiana na Show hiyo. Ni kwamba Utepe umekatwa rasmi kuhusiana na Show hiyo ambayo ilikuwa ya kipekee miongoni mwa Shows ambazo zimewahi kufanyika Mkoani Mwanza.


Afisa Masoko JB Belemont Suleiman Kupaza (Kushoto) akizungumza juu ya Shows za Usiku wa Mwafrika. 

Kwanza unapaswa kufahamu kuwa shows hizo zitakuletea burudani za Kiafrika, Misosi ya Kiafrika na Mavazi ya Kiafrika ambapo atakaetokelezea Kiafrika atapata Zawadi. 

Jukwaani sasa ndipo kutakuwa na kasheshe, Hapa Saida Karoli pale Osogo Owinyo huku wakisindikizwa na Madancers wakali kutoka nchini Kenya ambayo wanafahamika kama Chipukizi.Com

Hakika ilikuwa balaa ukizingatia kwamba kiingilio kilikuwa ni sawa na bure ambapo Show ilivyoandaliwa. 

Pale JB Belemont Hotel VIP watalipa 20,000 na Viti vya kawaida ilikuwa 10,000 huku pale Buzuruga Plaza kiingilio kilikuwa ni 10,000.


Akizungumzia Shows hizo hii leo, Afisa Masoko kutoka JB Belmont Hotel Suleiman Kupaza amebainisha kwamba maandalizi yote yalikwisha kikamilifu ikiwa ni Pamoja na Wasanii waliotumbuiza katika Shows hizo kuwasili Jijini Mwanza na hivyo kuwasihi wakazi wa Jiji la Mwanza na vitongoji jirani waliojitokeza kwa wingi kushuhudia burudani ya kukata na shoka iliyodondoshwa siku hiyo ya Tarehe 01.08.2014 na tarehe 02.08.2014 ambapo Milango ilianza kufunguliwa mapema kabisa kuanzia majira ya saa moja jioni katika shows zote kwa maana ya JB Belmont na Buzuruga Plaza. 




Hawa ni Wasani kutoka nchini Kenya ambao wanafahamika kama Chipukizi.Com 


Hawa ni Wasani kutoka nchini Kenya ambao wanafahamika kama Chipukizi.Com 


Chipukizi.Com kutoka nchini Kenya 


Chipukizi.Com 


Huyu ndie Event Cordinatore mwenyewe, anafahamika kama Moses Manta.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: TAARIFA MPYA KUHUSIANA NA ZILE SHOWZ ZA USIKU WA MWAFRIKA ZILIZO FANYIKA JIJINI MWANZA. Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top