My Favourite Site

Blogger Tricks

widgeo.net
Designed by Jeymodel Fashion. Powered by Blogger.
Saturday, July 5, 2014

Hapo kwa mara nyingine napenda kuwapa shavu nene warembo wa nyumbani kwa kujua kujilipua popote wapatapo upenyo,

Hapo kwa mara nyingine napenda kuwapa shavu nene warembo wa nyumbani kwa kujua kujilipua popote wapatapo upenyo,


Si masihara kwani wanajiweza mno mno na kujitambua ni aina gani ya mavazi yanawatoa na kupendeza popote wapatapo mualiko. Kama hapo pichani ni warembo wa tz wakijinafasi, Kusema ukweli swala lavitenge kwa warembo wengi linawatoa swafi kuonyesha uzuri kila walichonacho kama uonavyo style tofauti za nywele!


Lime ndo ndimu jamani, sasa ipo rangi ya ndimu haswaa ile ndimu ambayo haijaiva ndo rangi ambayo imetufungulia mwaka huu katika rangi kama ilivyokuwa rangi pink mwaka jana. Najua utakuwa umepishana wajanja wameitinga au kuona madukani vitu viingi vikiwa vimegubikwa na hii rangi kama pochi, tops, heren, sketi , skafu na viatu pamoja na pamba kibao za kike na mashati pia ya kiume. Rangi hii nakumbuka enzi silee nipo shule ya msingi ilikujaga lakini tulikuwa tunaziita crazt color kutokana na mng’ao wake, na zilikuwa rangi mbili kama ilivyo lime na hii rangi ya machungwa maarufu kwa sasa kama Bambucha!! Haya mabinti ili ufanane na mjanja na uende na wakati huna budi ya kusaka kivazi kama sio viatu , pochi au chochote upendacho ili kabati lako lifanane na wenzio wanaoenda na fashion. Hata wewe kaisake mtu wangu!



Kwenye swala la majumba alimaarufu kama suti hapo nadhani nimewapa mlipuko wa maana

kama uonavyo pichana siku hizi suti si lazima sana iwe na rangi au kitambaa kiwe cha rangi moja bali hata nakshi au uchanganyaji wa rangi uwe wa ubunifu kweli kweli kama hapo pichani mzee mzima Will Smith akiwa kajilipuona na suti hiyo ya kama udongo udongo ama dark gold silk flani na mistari kwa mbali na shati la zambarau na tai ya silk zambarau na kitamba cha silk kifuani si masihara?




Hivi ni aina ya viatu ambavyo ni virefu kiasi chake ila kwa mabinti waliozoea kuvaaga mchuchumio hapo haitakuwa kazi sana kupata control ya kuvimudu hivi viatu!Tofauti yake hivi viatu na mchuchumio ni kwamba aina hii ya viatu pichani vina soli nene na pana sana.Uvaaji wa viatu hivi unapendezea sna kwenye majeans,minisketi,pensi nyanya.....gaucho....kapri inatoka bunduki kinoma!

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: Hapo kwa mara nyingine napenda kuwapa shavu nene warembo wa nyumbani kwa kujua kujilipua popote wapatapo upenyo, Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top