My Favourite Site

Blogger Tricks

widgeo.net
Designed by Jeymodel Fashion. Powered by Blogger.
Saturday, September 6, 2014

NAMNA YA SKAFU KATIKA KUIPENDEZESHA NGUO NA KUWA NA MUONEKANO WAKUVUTIA NA KUPENDEZA

NAMNA YA SKAFU KATIKA KUIPENDEZESHA NGUO NA KUWA NA MUONEKANO WAKUVUTIA NA KUPENDEZA



Skafu ni urembo unaoweza kuvaliwa na aina yoyote ya nguo iwe ni vazi la kawaida au suti ya aina yoyote. Skafu inawezesha nguo kuonekana ya kuvutia hata kama nguo ni ya kawaida kabisa. Skafu zipo za aina nyingi kama pashmina(mitandio), ndefu nyembamba, za mraba n.k.


Uvaaji wa Skafu



Skafu inaweza kuvaliwa katika mitindo mbalimbali kutokana na umbo lake na mvaaji anataka kuivaa vipi. Skafu inaweza kuvaliwa shingoni, kiunoni kama mkanda au kichwani kama kibanio au kufunika nywele. Skafu kubwa kama pashmina unaweza uitumia kujifunika hasa wakati wa baridi.


Ufungaji wa skafu shingoni


Skafu yenye umbo la mraba unaweza kuikunja kupata pembetatu kisha ukafunga pembe mbili nyuma ya shingo ili ule upande mpana uwe umelala kifuani chini ya shingo.
2.Skafu ndefu nyembamba inavaliwa kwa kuining’iniza shingoni na kuifunga na pini kwa mbele.Unaweza tumia ‘brooch’ au pete maalumu.


3.Skafu ndefu pia unaweza kuivaa shingoni upande mmoja ukining’inia kwa mbele na mwingine ukining’inia kwa nyuma.
4.Pashmina skafu unaweza kuivaa kwa kuikunja nusu na kuiweka shingoni kisha kuchukua upande mmoja na kuuweka ndani ya upande mwingine kama unafunga kamba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: NAMNA YA SKAFU KATIKA KUIPENDEZESHA NGUO NA KUWA NA MUONEKANO WAKUVUTIA NA KUPENDEZA Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top