My Favourite Site

Blogger Tricks

widgeo.net
Designed by Jeymodel Fashion. Powered by Blogger.
Tuesday, October 7, 2014

REDD'S SPORT DAY BONANZA, THIS IS HOW IT WENT DOWN

 REDD'S SPORT DAY BONANZA, THIS IS HOW IT WENT DOWN

Ilikuwa Jumapili tulivu katika kambi ya Redds Miss Tanzania 2014. Kama kawaida warembo waliamka na kujiandaa kwa ajili ya kukabiliana na ratiba ya siku hiyo.




Ilikuwa Jumapili tulivu katika kambi ya Redds Miss Tanzania 2014. Kama kawaida warembo waliamka na kujiandaa kwa ajili ya kukabiliana na ratiba ya siku hiyo.







Katika vitabu vyao vya kumbukumbu siku hii ilikuwa mahsusi kwa ajili ya Redds sports bonanza, tamasha la michezo la Redds lililofanyika Escape one kwa ajili ya kuchangisha fedha ambazo zitatumika kutoa misaada kwa wale wenye uhitaji.







Michezo mbalimbali ilifanyika ikiwemo ya kuruka, kuogelea, kukimbia mita 100, mchezo wa magunia, volleyball n.k.







Washindi katika michezo hiyo walikuwa Jihan Dimachk (Dar City Centre) aliyeshinda katika mchezo wa kuogelea, Naomi Kisaka (Dar City Centre) aliyebuka kidedea katika mchezo wa kuruka huku Elizabeth Tarimo (Lindi) akishinda michezo miwili -- mchezo wa kukimbia mita 100 pamoja na mchezo wa magunia.







Elizabeth Tarimo ambaye pia aliibuka kama mshindi wa jumla na kujinyakulia taji la Redds top sports woman amejishindia ticket ya moja kwa moja kuingia nusu fainali ya Redds Miss Tanzania 2014.










Fainali za Redds Miss Tanzania zitarushwa moja kwa moja na StarTV Jumamosi trh 11/10/2014. USIKOSE.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Item Reviewed: REDD'S SPORT DAY BONANZA, THIS IS HOW IT WENT DOWN Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top